Monday, November 26, 2012

SHAROMILIONEA AFARIKI DUNIA


MSANII WA MAIGIZO NA MUIMBAJI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA(BONG FLEVA),HUSSEIN MKIETY 'SHAROMILLIONEA (PICHANI) AMEPATA AJALI MBAYA MAENEO YA MUHEZA KATIKA KIJIJI CHA LUSANGA MKOANI TANGA AMBAPO NDIO NYUMBANI KWAO NA KUPELEKEA KUPOTEZA UHAI WAKE
KWA MUJIBU WA WASANII WENZAKE AMBAO NI MWANADADA SHILOLE NA STEVE NYERERE( KWA WAKATI TOFAUTI) WAMETHIBITISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO LEO JIONI

CHANZO CHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO BADO HAKIJAJULIKANA

Saturday, November 24, 2012

MSANII WA FILAMU JOHN MAGANGA AFARIKI DUNIA

 RIP JOHN MAGANGA
Kwa mara nyingine tena wiki hii tasnia ya filamu imepoteza msanii mwingine baada tu ya kumaliza mazishi ya Mlopelo. Msanii John Maganga amefariki katika hospitali ya Muhimbili.  Taratibu za mazishi bado zinafanyika.

Ni hivi karibuni tu msanii huyu alisema kuwa amefungua Kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Jom Entertainment Co. Ltd, pia akaeleza kuwa alianza kuona kipaji chake tangia mwaka 2001 alipokuwa akifundishwa na msanii nguli wa filamu nchini Ndumbago Misayo 'Thea' ambaye alikuwa mwalimu wake wa maigizo wakati wapo kanisani pale Mwananyamala, baada ya hapo filamu ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Miracle of Love  ambayo ilifanya vizuri sana katika kumtambulisha kisanaa nchini. Mwaka 2008 alishauriwa na ndugu yake Deogratias Shija kufungua kampuni yake kwa ajili ya kuendeleza fani ya filamu, kazi ambazo ziko tayari ni Beautfuls aliyowashilikisha wasanii kama Aunt Ezekier, Haji Salumu 'MBoto' na wengine wengi
Mungu aiweke pema roho ya msanii huyu ambaye ameondoka wakati anaanza kuchipua.

Saturday, November 10, 2012

Barabara kuu (super highway) ya Nairobi kwenda Thika imefunguliwa rasmi jana na Rais Kibaki. Je, unahisi Bongo tutaweza kuwa na barabara kama hii? Kama ndiyo, lini?

Barabara kuu (super highway) ya Nairobi kwenda Thika imefunguliwa rasmi jana na Rais Kibaki. Je, unahisi Bongo tutaweza kuwa na barabara kama hii? Kama ndiyo, lini?

Thursday, November 1, 2012

UZINDUZI WA BARABARA YA MKUU ROMBO-TARAKEA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kabla ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na washika dau wa miundombinu wakikata utepe  ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea  Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasin katika hafla ya ufunguzi rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.