Friday, October 19, 2012

BREAKING NEWZZZ

jijini Dar es Salaam hali si shwari  maeneo ya Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na Maktaba).

Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha shughuli nyingi kusimama.

Pichani ni maeneo ya Kariakoo magari ya jeshi JWTZ zaidi ya 8 yakiwa katika doria  maeneo ya Kariakoo.

Sunday, October 14, 2012

QN.Write a program that will print the contents of an array typed by the user in either ascending or descending order depending on the user`s choice.

import java.util.Arrays;
import java.util.Collections;

public class Djshark{

public static void main(String args[]) {
String[] companies = { "Google", "Apple", "Sony" };

// sorting java array in ascending order

printNumbers(companies);
Arrays.sort(companies);
System.out.println("Sorted String Array in ascending order : ");
printNumbers(companies);

// sorting java array in descending order

printNumbers(companies);
Arrays.sort(companies, Collections.reverseOrder());
System.out.println("Sorted int Array in descending order : ");
printNumbers(companies);

}

public static void printNumbers(String[] companies) {
for (String company : companies) {
System.out.println(company);
}
}

}

Thursday, October 4, 2012

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 06.10.2012 kuanzia saa 8 mchana. Pamoja na mambo mengine Kiongozi huyo wa CDM pia atatumia mkutano huo kuzindua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya daraja mbili,uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vilivyopo mtaa wa NDARVOI.

Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo unaotarajiwa kuwa gumzo.

Taarifa za awali zinasema mkutano huo pia utatumika kufuta nyayo za chama cha CUF ambacho kilisomba watu Dar-es-Salaam kwenda kuwahutubia Arusha ili kuepuka aibu ya kukosa watu.Pia inadaiwa wananchi wa Arusha wamedhamiria kuonyesha dunia uungaji mkono wao kwa chama cha CDM.

Wednesday, October 3, 2012

BUS LA DAR EXPRESS LAWAKA MOTO NJIAPANDA YA TANGA (SEGERA)

Basi la  Dar Express limepata ajali ya kuungua moto jana asubuhi katika njia panda ya Dar, Arusha, Tanga (Segera) hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha. Katika ajali hiyo mizigo yote iliteketea kwa moto huo ambapo abiria wengi waliokuwamo kwenye gari hilo walikuwa ni wanafuzi. lilitokea Rombo mkoani kilimanjaro.