Thursday, May 17, 2012

Hili ndilo Gari alilopatanalo ajali marehemu Patrick Mafisango maeneo ya TAZARA jijini Dar. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.

Kabla ya  kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.
Mwenyezi Mungu ilaze mahali pema peponi roho ya marehemu Patrick Mafisango.

Mchezaji Patrick Mafisango wa Simba afariki dunia

Mchezaji wa kimataifa Patrick Mafisango wa Simba SC
MCHEZAJI Patrick Mafisango wa timu ya Simba ya Dar es Salaam amefariki dunia leo kwa ajali ya gari katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Taarifa ambazo zimetolewa kutoka Klabu ya Simba zimesema Mafisango amefariki dunia leo asubuhi kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara. Mtandao huu utawaletea taarifa zaidi za tukio hilo muda mfupi baadaye. Mtandao huu pia unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na klabu nzima ya Simba kwa pigo hilo.